Enter Adress

Friday, November 9, 2012

HIKI NDICHO NILICHO KIGUNDUA KWENYE UCHAGUZI WA URAIS WA MAREAKANI

TUANZE NA PENZI , KWENYE MAFANIKIO HUWA PENZI LINA CHANUA KAMA UNAVYO JIONEA


 


 KWA UPANDE WA FAMILIA




NA HAWA NI WAFUASI WA OBAMA





KWA UPANDE WA ROMNEY HALI ILIKUWA HIVI




NA KWA UPANDE WA FAMILIA YA MR ROMNEY HALI ILIKUWA HIVI




NA HAWA NI WAFUASI WA ROMNEY






Monday, November 5, 2012

HATA KAMA TUNATOFAUTIANA KIMAWAZO KUPONGEZANA NI KITU KIZURI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe kwa hotuba nzuri ya kumkaribisha na kumsifia kwa kazi anayofanya katika maendeleo ya miundombinu nchini katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai.











Tuesday, October 30, 2012




Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti itakayokuwa inajulikana kama www.misstanzaniatreasures.com mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti hiyo, Bw. Ali Zoeb (kushoto) na mshauri wa habari wa tovuti hiyo, Bw. Peter Keasi.

MISS TANZANIA YAZINDUA TOVUTI YASISITIZA UMUHIMU WA UREMBO



Jamii imesisitizwa kuona shughuli za urembo kama fani nyingine ambayo ikifanywa vizuri inaweza kumkomboa mshiriki kiuchumi na kumuibua kama mtu wa muhimu katika jamii.

Wito huu umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel aliyekua mgeni rasmi katika uzinduzi wa tovuti ya mashindano hayo, www.misstanzaniatreasures.com, mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
“Lengo la tovuti hii ni kutaka kueneza elimu hiyo na kuonyesha kwamba urembo ni kazi au fani kama nyingine na wala haina uhusiano wowote na uhuni kama baadhi ya watu wanavyoendelea kuamini,” alisema Bw. Prashant.
Alisema wengi wa warembo waliowahi kufanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania leo hii ni watu wenye mafanikio makubwa, kila mtu akifanya kile anachokipenda na kukiweza. 
Alisema tovuti hiyo inataka kuwaibua siyo tu washindi wa Miss Tanzania waliopita, bali washiriki mbalimbali waliwahi kushiriki katika mashindano hayo na kuonyesha wako wapi, wanafanya nini, ndoto na matarajio waliyonayo na hata changamoto wanazokumbana nazo.
Hadi sasa kuna jumla ya washiriki zaidi ya elfu tano tangu Miss Tanzania ianzishwe mwaka 1994. 
Alisema kamati ya MissTanzania inaamini warembo hawa ni hazina na hivyo wanataka kuonyesha hazina iliyopo katika taifa.
Alisema juhudi hizi za kuanzishwa kwa tovuti hii zitafuatiwa na uanzishwaji wa jarida litakalojulikana pia kama Miss Tanzania Treasures.
Akielezea zaidi alisema sehemu ya faida itakayotokana na tovuti hii na jarida hilo itatumika katika kuchangia maendeleo ya warembo hawa kama elimu na shughuli mbalimbali wanazofanya kwa utaratibu utakaopangwa.  Pia, faida itakayopatikana itatumika katika kusaidia watoto yatima hapa nchini.
“Tovuti hii itasaidia dunia nzima kushuhudia na kujua kwa undani kuhusu Miss Tanzania.  Hii ni fursa nyingine katika kukuza sekta ya utalii hapa nchini maana hakuna ubishi kwamba Miss Tanzania imekua moja ya njia za kukuza utalii wetu nje ya nchi,” alisisitiza.
Akielezea zaidi alisema tovuti ni njia muafaka katika kipindi hiki cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo maendeleo yanategemea zaidi ufanisi katika mawasiliano.
“Tovuti hii itasaidia kujenga mtandao baina ya warembo wenyewe na wakajua jinsi ya kushirikiana katika maswala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi na hivyo kuchochea maendeleo,” alisema.
Alisisitiza kuwa tovuti hii pia itasaidia kujenga mahusiano na mawasiliano kati ya warembo wa Miss Tanzania kwa upande mmoja  na wadau wa maendeleo ndani na nje ya nchi.
“Tutawashirikisha wadau mbalimbali katika swala hili muhimu na ni wito wetu kwamba wasituangushe kwa faida ya nchi yetu,” alisema Bw. Prashant.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti hiyo, Bw. Ali Zoeb aliwaahidi warembo walioshiriki uzinduzi huo kuwa tovuti hiyo itasaidia sana katika kuwaunganisha na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi na kuwasisitiza warembo popote walipo kuanza kujenga mazoea ya kutembelea tovuti hiyo na kujua kinachojiri.

Naye, mshauri wa habari wa tovuti hiyo, Bw. Peter Keasi alisema tovuti na jarida litakaloanzishwa hivi karibuni vitasaidia kurahisisha mawasiliano kufanya kazi kama daraja baina ya warembo hapa nchini, jambo alilosema ni muhimu kwa maendeleo.

Uzinduzi huo ulishuhudiwa na warembo walioko kwenye kambi ya Miss Tanzania kwa sasa pamoja na wadau wengine wa urembo hapa nchini.

Mwisho

Friday, October 26, 2012

NAIBU WAZIRI AELEZA KILICHOMFANYA KUSEMA TANZANIA NI MUUNGANIKO WA ZIMBABWE NA PEMBA



Naibu Waziri Philipho Mulugo
Kuanzia juzi taarifa na video ya Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi wa Tanzania Philipo Augustino Mulugo zimeanza kusambaa kwa watanzania wengi kuhusu alichosema akiwa Afrika Kusini kwenye mkutano wa kimataifa  kwamba Tanzania ni muungano wa visiwa vya bahari ya Hindi, Pemba na Zimbabwe.

Mulugo leo amezungumza na Power Breakfast ya CLOUDS FM na kusema kabla ya yeye kupanda kuanza kuzungumza kulikua na kiongozi wa Zimbabwe ambae alitoka kuzungumza na nina mkariri akisema

 “sasa ilibidi lazima baada ya kufika pale ni lazima umshukuru mwenzako aliepita sasa kama mawazo ndiyo yaliyokua yamedhania hivyo kwamba basi hapa naitamka Zimbabwe kwa sababu zote zimeanzia na Z labda ilitokea hivyo lakini nakiri kabisa kwamba sikua na makusudio kwamba naitamka Zimbabwe lakini kule kwenye power presentation inaonekana kabisa ukifungua pale ni Tanzania imeungana na Zanzibar Pemba na Tanganyika kama ambavyo tunajua kwa sababu ile ni historia hakuna asiejua hata mtoto wa darasa la tatu”

“Niseme tu kwamba hiyo ni kuteleza kwa ulimi na nilikua namfikiria yule waziri wa Zimbabwe kwa sababu alikua ametoka kuhutubia kabla ya mimi, nilikua naomba ieleweke hivyo………… 

na wengi wameongea wanahoji lugha kiingereza, jamani tukubaliane kwamba kusema Zimbabwe badala ya Zanzibar sidhani kama inaendana na drama yenyewe kwa sababu mimi nimekua mwalimu mda mrefu nimefundisha wanafunzi wangu na wananifahamu uwezo wangu mkubwa na tena mimi ni mwalimu wa historia hata degree yangu ni mimi ni mwalimu wa historia na Economics, 

labda niliongea nilikua sijielewi na ningegundua nimetamka Zimbabwe ningeweza kuomba radhi, mataifa yote wawe waafrika wawe wazungu wengi huwa tunazingatia kuangalia kwenye power point pale, wengi huwa hawasikilizi sauti” – Mulugo

Kuhusu kukosea kutaja mwaka, Namkariri naibu waziri akisema “mimi pale nia yangu ilikua ni kusoma namba moja moja  nikashtukia nakwenda kusoma mbili, haijakaa kama nimekosea kiingereza kama watu wanavyoipanua kwa mfumo huo lakini kama watu wamenielewa hivyo niombe tu msamaha”(SOURCE djfetty.blogspot.com)