Watu mbalimbali duniani wamepokea kwa hisia tofauti hatua ya serikali ya Pakistan kumhukumu kifungo cha miaka 33 jela daktari maarufu nchini humo Shakeel Afridi baada ya kutiwa hatiani kwa uhaini.
Baadhi
ya majirani wa daktari huyo nchini Pakistan wamesema adhabu aliyopewa
ni ndogo kutokana na vitendo vyake vya kulisaliti taifa lake kwa maslahi
ya serikali ya Marekani. Marekani nayo inasema haioni sababu za
serikali ya Pakistan kumfunga Afridi kwa vile hana hatia.
Afridi
anatuhumiwa kuwapatia taarifa maafisa wa shirika la ujasusi la
Marekani, CIA zilizosaidia kukamatwa na kuuawa kwa kiongozi wa kikundi
cha kigaidi cha Al-Qaeda, Osama Bin Laden mjini Abbottabad nchini
Pakistan alikokuwa akiishi na familia yake.
Serikali
ya Pakistan imedai kuwa daktari huyo alijidai kufanya kampeni ya chanjo
ya Polio nchini humo lakini badala yake alitumia kampeni hiyo kufanya
uchunguzi na kujua mahali alipo Osama na kisha kutoa taarifa kwa CIA
walioshambulia eneo hilo na kumuua.
No comments:
Post a Comment