Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Msata – Bagamoyo na kuwataka wakazi wa mkoa wa Pwani kutumia fursa zinazotokana na barabara hiyo kujiletea maendeleo.
Rais
Kikwete amesema barabara hiyo itakapokamilika ujenzi wake kwa kiwango
cha lami itafungua milango ya biashara kwa wakazi wa mkoa wa Pwani
pamoja na kupungunza tatizo la foleni katika barabara ya morogoro.
Rais
Kikwete aliwasili katika kijiji cha kiwangwa kuweka jiwe la msingi
ujenzi wa kilometa 64 za barabara ya msata –bagamoyo kwa kiwango cha
lami na akatumia fursa hiyo kuwaasa wakazi wa mkoa wa Pwani kutumia
barabara hiyo kujiletea maendeleo.
Halikadhalika
Rais Kikwete amezungumzia tatizo la watu wanaovamia na kujenga nyumba
katika hifadhi ya barabara kuwa katu hawatalipwa fidia na badala yake
watakaolipwa fidia ni wale tu ambao watabainika kuwa barabara iliwakuta.
Mapema
akimkaribisha Rais Kikwete kwenye sherehe hizo, waziri wa ujenzi Dokta
John Magufuli ameiomba bodi ya wakandarasi nchini kuichukulia hatua
kampuni iliyopewa zabuni ya kufanyia tathmnini ujenzi wa barabara hiyo
kwa kuifanya kwa kiwango cha chini jambo ambalo limeisababishia serikali
hasara kubwa.
Mkuu
wa wakala wa ujenzi wa barabara nchini injinia Patric Mfugale amesema
ujenzi wa kilometa 64 za barabara ya Msata Bagamoyo unagharimu shilingi
bilioni 90 fedha ambazo zimetolewa na serikali ya Tanzania ambapo hadi
sasa kilometa 37 zimekamilika.
No comments:
Post a Comment