Waziri wa viwanda, biashara na masoko Dkt.Abdala Kigoda amefungua maonyesho ya saba ya biashara ya afrika mashariki yanayofanyika jijini Mwanza.
Katika
ufunguzi huo, Waziri kigoda amebainisha azma ya nchi za jumuiya ya
afrika mashariki ya kuanzisha vituo maalum vya ukaguzi wa bidhaa katika
maeneo ya mipaka ili kuwaondolea wafanyabiashara upotevu wa muda na
usumbufu wanaoupata hivi sasa wanaposafirisha bidhaa zao kutoka nchi
moja kwenda nyingine.
Dkt.Kigoda
amesema kuwa vituo hivyo vitakavyojulikana kwa jina la one border post
center vitawawezesha wafanyabiashara wanaoingiza ama kutoa bidhaa zao
nchini kukaguliwa katika kituo kimoja pekee tofauti na sasa ambapo
wafanyabiashara wanakumbana na vikwazo mbalimbali vikiwemo idadi kubwa
ya vizuizi vilivyoko barabarani.
Ni
maonyesho ya saba ya biashara ya afrika mashariki yanayofanyika jijini
mwanza na kushirikisha makampuni na taasisi mbalimbali za kibiashara
kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania.
Waziri
Kigoda pia ameletoa rai kuwa maonyesho hayo yatumike kuondoa dhana
potofu iliyojengeka miongoni mwa wananchi kuwa bidhaa bora ni zile
zinazotoka nje ya jumuiya ya afrika mashariki.
Maonyesho
hayo yanayozishirikisha zaidi ya makampuni mia nne kutoka ndani na nje
ya nchi yanatarajia kufikia tamati Septemba tisa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment